Watu 20 Wanashikiliwa na Polisi kwa Kukutwa Wakifundishana Kufanya Mapenzi ya Jinsia Moja - bongo specially

Breaking

Post Top Ad

Saturday 16 September 2017

Watu 20 Wanashikiliwa na Polisi kwa Kukutwa Wakifundishana Kufanya Mapenzi ya Jinsia Moja


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi-Unguja linawashikilia watu 20 kwa tuhuma za kukutwa wakifundishana kufanya mapenzi ya jinsia moja.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharib Hassan Nassir amesema watu hao wamekamatwa wakati wakipatiwa mafunzo ya namna ya kuzitambua haki zao yaliyokuwa yakitolewa na taasisi iliyotambulika kwa jina la Bridge Initiative.

Hata hivyo hatua hiyo imekuja mwezi mmoja baada ya kauli ya mkuu wa mkoa huo ambaye pia ndio mwenyekiti wa ulinzi na usalama RC Ayoub Mahamoud kutamka kukomesha vitendo hivyo mara moja ambavyo vinaiharibu sifa ya Mkoa huo.

Mabli na hilo mkuu huyo wa Mkoa akiliongoza Jeshi la Polisi tayari yuko katika operesheni ya kuzidhibiti biashara ya Dawa za kulevya, ambapo zaidi ya Vijana 50 mkoani humo walikubali kuachana na matumizi ya dawa hizo.

No comments:

Post a Comment