Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo alimaarufu kama Mzee wa Upako amefunguka na kusema watu wasichukulie tatizo lililompata Tundu Lissu kupigwa risasi kama njia kujipatia umaarufu wa kisiasa na dini.
Mchungaji Lusekelo ameandika ujumbe huo kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii na kusema kuwa mbona watu hao hawakuonekana kulaani mauaji ya Kibiti au kuitisha maombezi baada ya watu Kibiti kuuawa.
"Tusitumie tatizo la ndugu yetu Tundu lissu kujipatia umaarufu wa kisiasa au wakidini, mtu yeyote ambaye anatumia tukio hili kujipatia umaarufu wa kisiasa au wakidini namfananisha na wale wahuni ambao basi likianguka anaenda kuchukua simu kwanza, ni jambo ovu sana wewe unakuwa ni sehemu ya watu walio mpiga risasi Tundu lissu. Mwenzako anaumwa wewe unatumia ugonjwa wake kujipatia umaarufu wa kidini au wakisiasa ni jambo baya sana, mbona sikusikia wakilaani mauaji ya kibiti au kuitisha maombezi watu wakibiti walipo uwawa, mbona hawaja laani utekaji na mauaji ya watoto Arusha hata wa Marekani (umoja wa ulaya) sikusikia wanalaani mauaji ya kibiti" aliandika Mzee wa Upako
Aidha Mchungaji huyo amesema kuwa yeye anaamini watu hao wanatumia matatizo ya Tundu Lissu kujiongezea umaarufu wa kisiasa na kidini "Najua wanatumia matatizo ya Tundu Lissu kujiongezea daraja la umaarufu la kisiasa au kidini. Natumia lugha ya kibantu ni Mwiko, ni mwiko tubaki kuwa wamoja tuviachie vyombo vya dola vifanye kazi yake" Alisisitiza Mzee wa Upako.
Mzee wa Upako amesema maneno hayo baada ya Jumapili Mchungaji Gwajima kufanya maombezi maalum kanisani kwake Ufufuo na Uzima kwa ajili ya kumuombea Tundu Lissu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana, lakini pia baada ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kutoa taarifa ya kulaani tukio la Tundu Lissu kushambuliwa na risasi na watu wasiojulikana akiwa mjini Dodoma Septemba 7, 2017.
No comments:
Post a Comment