Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Gabriel... kumshauri Rais Magufuli aivunje Halmashauri ya Mbeya - bongo specially

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 13 September 2017

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Gabriel... kumshauri Rais Magufuli aivunje Halmashauri ya Mbeya



Halmashauri ya Mbeya imepewa miezi mitatu kubadili mwenendo wake wa kutoa maamuzi yasiyofuata kanuni, taratibu na sheria, kwa maelezo kuwa yamekuwa yakiingizia serikali hasara ya mamilioni ya shilingi ambapo mkuu wa mkoa Amos Makala pia ameonya kuwa ikiwa itashindwa kujirekebisha atashauri mamlaka husika kuichukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuivunja.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Gabriel Makala amefikia hatua hiyo baada ya uongozi wa halmashauri ya Mbeya , kudaiwa kukaidi ushauri inaopewa na viongozi wa serikali na kutoa uamuzi mbovu, ikiwemo kuwafukuza kazi watumishi wanne bila kufuata taratibu, hivyo kupelekea watumishi hao kukata rufaa kwenye tume ya utumishi wa umma, na kushinda rufaa hiyo, ambapo tume imeamuru warejeshwe kazini na walipwe stahiki zao.

Aidha Mkuu wa mkoa pia amewaonya baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo, a kujihusisha na siasa kutoa taarifa za upotoshaji kwa madiwani ambazo ndizo zinasababisha kutolewa kwa uamuzi ambayo si sahihi.
Mwalingo Kisemba ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya anasema halmashauri yake ilitimiza wajibu wake na kwamba kushinda rufani ni sehemu ya utaratibu na ni haki ya mtumishi na kwamba halmashauri yake haina tatizo na uamuzi huo.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Agosti mwaka huu alifanya ziara Mkoani Mbeya na kuitadharisha halmashauri ya wila ya Mbeya kuwa uamuzi wake wa kuwafukuza watumishi bila kufuata taratibu inaweza kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya zaidi ya shilingi milioni 400.

No comments:

Post a Comment